Unyama! Jamaa anayedaiwa kuwauwa wanawake na kukata sehemu zao nyeti ashikwa -Isiolo

Jamaa anayedaiwa kuwa muuwaji  wa wanawake katika kaunti ya Isiolo na kukata sehemu zao nyeti ametiwa mbaroni na maafisa wa usalama.Anaidaiwa kuwa baada ya kukata sehemu hizo za wanawake alikuwa anazika katika maeneo tofauti ya kaunti hiyo.

Kulingana na maafisa wa polisi kaunti hiyo ya Isiolo,miili ya waathiriwa na ambao waliuwawa na mshukiwa imepatikana katika eneo la Bulapesa na  Wavera huku uchunguzi mwengine ukiendelea kufanyika.

Mkuu wa polis kaunti hiyo Harm Shambi amesema ni sharti wananchi wa kaunti hiyo washirikiane kwa kutoa taarifa kwa asasi kuu za serikali ili kufanikisha mchakato wa familia zilizoathirika kupata haki.

Mshukiwa alitiwa mbaroni akiwa mafichoni eneo la Timau kaunti ya Meru kabla ya kupelekwa kwa kituo cha Isiolo ambapo anasubiri kufikishwa mahakamani.