Unyama! Msichana kubakwa kisha mwili wake kutupiwa asidi

Ni unyama ambao msichana wa miaka,14, aliweza kupitia baada ya kukumbana na kifo chake.

Imekuja katika mawazo ya kila mwananchi kuwa mwanamke yeyote akipotea atapatikana akiwa ameaga dunia.

Msichana huyo aliweza kufa kifo cha uchungu mwingi.

Wanawake wanne wameweza kukamatwa baada ya msichana wa darasa la saba kubakwa, na mwili wake kumwagiliwa asidi kisha kuuwawa eneo la Eastliegh kaunti ya Nairobi.

Walio mikononi mwa polisi ni mwanafunzi wa miaka 28 shangazi Nathifa Mohamed.

"Inashukiwa kuwa msichana huyo aliweza kubakwa na kuuwawa nyumbani alipokuwa anaishi na shangazi yake Nathifa Mohamed," Alisema mwanaharakati Florence Kanyua.

Polisi walisema kuwa wanaume, wanawake na watoto kadhaa walikuwa katika nyumba hiyo wakati msichana huyo alipokuwa akiuwawa.

Msichana huyo aliweza kupotea kwa siku nne baada wa mwili wake kupatikana Jumamosi.

"Watoto waliweza kusikia arufu mbaya kabla ya kuona mwili huo ambao ulikuwa umeoza sebuleni mwa nyumba hiyo,

"Kisha walikimbia na kuja kutuambia kisa hicho," Alieleza jirani.

Shangazi Nashifa aliweza kuutoa mwili huo mahali pake pa siri pa kuzikwa. Polisi waliweza kuteka mwili huo katika msikiti wa South C wakati ulipokuwa amepelekwa na ambyulensi.

"Mwili huo ulikuwa umesafishwa tayari kufanyiwa mazishi," Mchunguzi alisema.

Majirani walisema kuwa msichana huyo amekuwa akiishi na shangazi yake Nashifa Mohamed na wanawake wengine watatu.

Polisi walisema kuwa washukiwa hao ni wa asili ya somali."Msichana huyo ni mkenya bali watatu hao ni wageni," Polisi alisema.

Washukiwa hao walidai kwa polisi kuwa msichana huyo alikufa kwa ajili ya ugonjwa wa moyo, lakini majirani walisema kuwa wanaume walikuwa wanakuja mara kwa mara katika nyumba hiyo lakini hawakuweza kuruhusiwa kuingia.

"Kulikuwa na wanaume na watoto katika nyumba hiyo, tunaweza kutafuta wanaume hao lakini watoto hao wako mahali kuna usalama ili waweze kutoa ushahidi wao,

"Mwili huo ulikuwa umeoza majeraha ya asidi ni ushaidi kuwa msichana huyo alipitia kiwewe siku hizo nne alipokuwa ametoweka," Alieleza polisi.

Nashifa aliweza kukamatwa siku ya Jumapili na kisha kuenda mahakamani Jumatatu. Polisi waliona ni vyema kumuweka rumande  katika kitua cha polisi cha Pangani kwa siku 14 wakiendeleza uchunguzi wao.

Washukiwa wale wengine wanatarijiwa kuwa mbele ya mahakama hivi leo, msichana huyo aliweza kuzikwa Jumatatu katika makaburi ya Lang'ata kama ulivyo utamaduni wa kiuslamu.