Unyama ulioje? Mfanyibiashara auliwa na wanawe wawili kubakwa Bungoma

Mfanyibiashara maarufu wa soko la Chebukwabi  eneo bunge la Kimilili kaunti ya Bungoma ameuliwa kwa kupigwa risasi  na majambazi sugu huku mwanawe mmoja wa kiume pamoja na bintize wawili wakiuguza majeraha baada ya kubakwa kwenye tukio hilo.

Akizungumza na wanahabari  kutoka hospitali ymoja ya kibinafsi anakouguza jeraha ya risasi miguuni, mwanawe marehemu Eric Wafula Barasa amesema babake alipigwa risasi mwendo wa saa sita usiku mda mfupi tu baada ya kuwasili kutoka sokoni anakofanyia biashara.

Amesema juhudi zao za kujinasua hazikufua dafu huku dadake zake  wawili wakinajisiwa na genge hilo kwa takribani masaa mawili huku maafisa wa polisi wa kambi ya chebukwabi wakidaiwa kuchelewa kuwasili mahali pa tukio hilo.

Hata hivyo, wanasiasa wa eneo hilo wakiiongozwa na Didmus Baraza na Aggrey Mulongo wameshtumu tukio hilo na kuomba kamishna wa kaunti ya Bungoma Joshua Chepchieuhang kuhrakisha uchunguzi la sivyo waandae maandamano dhidi ya vitengo vya usalama vya eneo hilo.

Hakuna mshukiwa yeyote aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo.