Kulingana na polisi hao, mwanamke huyo alikuwa anaendesha gari hilo akielekea Loitoktok alipoamua kukiuka amri zao.
Mkuu wa polisi kaunti ya Kajiado Beatrice Gachago amesema maafisa wa usalama eneo hilo walikuwa wamepokea taarifa kuhusiana na gari lililokuwa limeibwa. Gachago ameongezea kuwa gari alilokuwa analiendesha mwanamke huyo lilikuwa linafanana na lile walililokuwa wanatafuta maafisa hao.
Walioshuhudia kisa hicho wanasema mwanamke huyo alikuwa analiendesha gari hilo akielekea eneo la kizuizi na alipoambiwa asimame akakataa, jambo lililowafanya polisi kumfyatulia risasi.
Kwa sasa mwathiriwa amelazwa katika hospitali ya Makindu akiuguza majera ya risasi tano, taarifa ambazo zimethibitishwa na mkuu wa afya katika hospitali hiyo ya Makindu David Kasanga.