Polisi huko Makueni wanamsaka mwanamume mwenye umri wa miaka 35 ambaye alimuua babake kwa kutumia mshale na kisha kuuteketeza mwili wake katika kijiji cha Masalani.
Mshukiwa aliyetambuliwa kama Nicholas Katua pia alimjeruhi kakake wa kambo katika mzozo huo wa ardhi kabla ya kuiteketeza nyumba yake.
Baadaye mshukiwa alitoroka eneo la tukio na bado hajakamatwa.