UNYAMA!!!Mwanaume amuua mwanawe,3, kwa kujoa kitandani

kenya-police-e1578832389578
kenya-police-e1578832389578
Polisi wa Kituo cha polisi cha Webuye katika kaunti ya Bungoma wamemtia baroni mwanaume mmoja baada ya kumchapa mwanawe wa kambo hadi kufa baada ya kukojoa kitandani.

Mashahidi walioongea na wanahabari walisema kuwa mwanaume huyo alimchapa mwanawe kichapo cha mbwa Alhamisi asubuhi na mapema na kumuacha kando ya barabara.

Baada ya kichapo hicho mtoto huyo alibaki na majeraha, na kuaga dunia kwa ajili ya majeraha hayo aliopata kutokana na kichapo hicho.

Wakaazi wa eneo hilo walimtia  mwanaume huyo  adhabu kwa kitendo hicho lakini polisi waliwasili kwa mapema kabla ya kuchapwa.

Polisi wamemshika mshukiwa huyo wakati uchunguzi wa kisa hicho unapoendelea, na mwili wa mwendazake kupelekwa katika chumba cha kuifadhi maiti cha Webuye.