Uongozi wa Idi Amin! Tazama kituo cha kuweka watu kwenye Karantini Busia

EW6h0jDX0AEEQB6
EW6h0jDX0AEEQB6
NA NICKSON TOSI

Baada ya taifa la Kenya kuamua kuanzisha ugatuzi nchini,wakenya walikuwa na matarajio kuwa huenda hatua hiyo ingeleta uongozi karibu na hivyo kupata huduma bora tofauti na ilivyokuwa inawalazimu kusubiri kutoka kwa serikali kuu.

Uongozi wa gavana wa Busia Sospeter Ojamong haustahili kupewe heshima kamwe na hautofautiani kabisa na kiongozi wa zama wa Uganda Idi Amin Dada.

Yamkini si mara ya kwanza kwa wakaazi wa gatuzi hilo kulalamikia uongozi butu, miundomsingu duni na ufisadi uliokita mizizi, huku serikali hiyo ikiendelea kuyatupilia malalamishi ya wakaazi wa Busia katika kaburi la sahau.

Tafakari haya, mwanamke mmoja na mwanawe wa mwezi mmoja aliwekwa kwenye chumba ambacho hakikuwa na kitanda wala mtoo wa kumlalisha mwanawe kwa madai kuwa alikiuka amri ya kufika kwa nyumba saa 7 jioni.

Mama huyo alilazimika kumtandikia mwanawe katoni ili alale.

Tazama picha hizi.