Upekuzi : Je, kuna njama ya wabunge kumfanya Duale waziri mkuu?

Aden Duale
Aden Duale
Makala ya upekuzi imebaini kwamba kuna njama ya baadhi ya wabunge kufanyia marekebisho katiba na kumvisha Aden Duale madaraka ya Waziri Mkuu.

Hata ijapokuwa pendekezo la kurejesha afisi ya waziri mkuu lipo kwenye ripoti ya BBI, imebainika kwamba baadhi ya wabunge wamechangamkia jambo hili na wamo mbioni kuwasilisha bungeni marekebisho hayo ya kikatiba.

Mbunge mmoja aliiambia makala ya upekuzi kwamba mswada wa kufanyia marekebisho pendekezo hilo litawasilishwa juma lijalo.

na iwapi itapitishwa kuwa sheria basi Aden Duale ambaye ni mbunge wa Garissa mjini atakuwa waziri mkuu.

Wajibu wake mpya utakuwa ni kuongoza vikao vya mawaziri ambavyo kwa sasa vinaongozwa na Fred Matiangi.

Hata hivyo kuwa hofu kwamba huenda isipate uungwaji mkono mwafaka kutoka kwa wabunge wanaoekemea mrengo wa upinzani.