'Upendo ni wa kweli Uganda nashukuru,' Diamond Platinumz asema

Mwimbaji Diamond Platnumz alivutia umati mkubwa katika onyesho lililofanyika siku ya Ijumaa usiku katika mji mkuu wa Uganda, Kampala.

Diamond amekuwa nchini Uganda tangu siku ya Jumatano hadi Ijumaa, alipo utumbuiza umati mkubwa na nyimbo zake.

Diamond alichapisha kwenye mitandao ya kijamii alivyokuwa kuwa na furaha kwa upendo alioupokea kutoka Waganda akisema hakuwa anatarajia hayo kwani mpenziwe wa hapo zamani Zari ni mzaliwa wa Uganda.

Maonyesho ya Ijumaa yalikuwa ya kwanza kwa Diamond nchini Uganda tangu alipoachana na Zari mnamo Februari mwaka jana.

Soma mengi

https://www.instagram.com/p/B0alULwnOFs/