Upweke Mojawapo Ya Sababu Za Kusambaratika Kwa Ndoa Za Wanaoishi Maeneo Tofauti

Wanawake wanapoendelea kupewa uwezo na wanaume nao kujizatiti, kasumba kwamba mwanamke ni wa jikoni na kujifungua watoto inatokomea katika jamii.

Katika ndoa nyingi wanawake kwa wanaume wanalazimika kufanya kazi ikizingatiwa gharama ya maisha ilivyopanda. Kutokana na hili basi pengine USHAWAHI  kuacha mkeo au mumeo  katika eneo moja na uende kufanya kazi katika maeneo mengine ya nchi na hata ulimwengu.

Wengi watakwambia wakati kama huu mawasilaino ni muhimu, kweli kabisaa. Lakini mtaalam wa maswala ya uhusiano Sumi Mwai anasema juhudi zaidi zinafaa kuwekwa. Bi Mwai anasema kila mmoja anafaa kujukumika kuhakikisha kwamba ndoa na uhusiano wao unaboreka.

Anasema mara nyingi upweke na mahitaji yasiyotimizwa husababisha ndoa kama hizi  kusambaraqtika na hata watu kuachana. Ili kuepuka hil Bi Mwai anasema ni jukumu la mke na mume kuhakikisha kwamba anatimiza kila makubaliano watakayojiwekea katika uhusiano wao.

Kuna kasumba kwamba wanawake  ndio huvumila zaidi kuliko wanaume katika ndoa na uhusiano kama huu. Hata hivyo mtaalma Sumi anasema hili hutegemea tabia za mtu wala halina mume wala mke .