Urembo wa aina yake!Tazama picha ya mama mkwe wa Lulu Hassan

detkezylyp1jansr5b9610894fb52
detkezylyp1jansr5b9610894fb52
Rashid Abdalla na mke wake Lulu Hassan wamezoea kama ibada kuweka mambo ya familia yao mbali na mitandao ya kijamii kwani wanaelewa fika kuwa si vyema kumwaga mtama penye kuku wengi.

Hata hivyo,juzi Rashid Abdalla alimua kuweka picha ya mamake kwenye mtandao wa kijamii huku akiomboleza kifo cha ndugu yake.

Ukiangalia picha hii,utastaajabu kuona vile amabvyo wawili hawa wanafanana si kidogo.

Sote twajua kuwa mtangazaji Rashid ana uhusiano mzuri sana na wengi na kwa hivyo alivyoweka picha hii kwenye mtandao wa kijamii wengi walimtumia ujumbe wa kumtia moyo na kumwambia asitie shaka kwani mama yake atapona.