Usalama waimarishwa mjini Mombasa

Maafisa wa polisi wametumwa kulinda doria katika maeneo ya makanisa mjini Mombasa kufuatia tishio la ugaidi pwani ya Kenya. Maafisa hao wanajumusiha maafisa wa CID na polisi wa utawala.

Askofu wa kanisa la Kiangilikana Julisu Kalu pia ametoa wito kwa waumini katika sehemu za kuabudia kuwa macho na kupiga ripoti kwa maafisa hao kuhusu chochote wanachohisi kitatishia usalama wao.