'Usawa wa jinsia ilikuwa ndoto mbaya na kosa,'Moses Kuria

Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria Jumanne kupitia kwenye mitandao ya kijamii ya twitter alisema kuwa usawa wa jinsia ulikuwa kosa kubwa na ndoto mbaya ambayo inahitaji kutolewa kwenye katiba.

Huku akinakili ujumbe wake Kuria alidai kuwa njia moja wapo ya kusuluhisha usawa wa jinsia ni kubadilisha katiba kupitia bungeni.

Pia alisema kuwa ni ukweli ambao wakenya wanapasa kukabiliana nao na kama wabunge wako tayari kufanya mabadiliko ya usawa wa jinsia.

https://twitter.com/HonMoses_Kuria/status/1310795263561400320

"Suluhu la kipekee la usawa wakijinsia ni kubadilisha katiba kupitia bunge ili kuondoa hitaji la usawa wajinsia tuko tayari, ilikuwa makosa na ndoto mbaya huo ndio ukweli tunapswa kuutazama." Aliandika Kuria.

Ni ujumbe ambao uliibua hisia mseto kutoka kwa wekenya wengi na hizi hapa baadhi za hisia zao.

Selassie Souljah : Why is this country so afraid of having strong, sober minded women in positions of leadership!!! Look at where this country is courtesy of male leadership over the years.
 Frank Mtetezi (BAF) :So you are implying that Kenya doesn't need ⅔ Gender rule?
Rofi:It should be 50%! There should be total equality for men and women. On top of that, affirmative action for women. Why should men be treated more favourably than women?
Mihr Thakar: I find it difficult to imagine that you can change the constitution without a people's referendum.