Usidharau kazi ya mwenzako!Rashid Abdalla aeleza kwanini walikuwa wamevalia mavazi ya rubani na mkewe

Jumapili katika Nipashe wikendi habari ambazo usomwa na Rashid Abdalla na Lulu Hassan, waliwaacha wengi wakizungumza baada ya kusoma habari hizo za saa moja wakiwa wamevalia mavazi ya rubani kila mmoja.

Si mmoja au wawili bali watu na mashabiki kadhaa walipendezwa na mavazi hayo ya wanahabari hao wawili.

Hata hivyo mavazi hayo yalikuwa ya kuwaheshimu marubani ambao kazi zao zilisimama kwa ajili ya janga la corona, si kazi hiyo tu pekee ilhali kazi nyingi zimeadhirika na janaga hili.

Abdalla alizidi na kuzungumza na kusema kuwa watakuwa wakiheshimu sekta mbalimbali za uchumi ambazo zimeweza kuathirika.

“Leo hii ladba uko nyumbani na unatizama Nipashe Wikendi na unaona tumevalia Vazi la rubani. Kwanza ni kutoa heshima kwa sector zote ambazo zimeadhirika kwa njia moja ama nyingine na Covid-19. Lakini pia kipindi hiki cha Covid-19 tumepata nasafi ya kujifunza kwamba hakuna kazi isiyokuwa na maana. Usidharau kazi ya mwenzako kwamba yako inaumuhimu. Kila kazi ya mtu inathamani yake na mchango wake katika kusukuma gurudumu la maisha. Hivyo basi kila Jumapili tutakuwa tukitoa heshima na kukumbushana kuwa kwa pamoja tumaweza kutimiza malengo, hakuna bingwa wala sefu." Alieleza Rashid.

Lulu Hassan naye aliongeza kwa kusema haya;

"Kwa hivyo basi mtazamaji tumefika anga tua ya nipashe wikendi umekuwa nami rubani wako Lulu Hassan na mwenzangu Rashid Abdalla.”

Wawili hao uwaacha webgi wakitamani ndoa yao kwa mfano mwema ambao uwapa mashabiki wao katika ndoa yao.