Usikanyage Mombasa iwapo hutaki kufa kwa ajili ya corona - CAS Mwangangi

mercy
mercy
Wakaazi wa Mombasa wapo katika hatari ya kuaga dunia kwa ajili ya COVID 19 kuliko wale walio Nairobi.

Katibu wa utawala wa  Afya Dr Mercy Mwangangi amesema ingawaje  Nairobi na Mombasa zote zimeorodheshwa kama kaunti hatari kwa ajili ya idadi ya juu ya  visa vya  COVID 19, Mombasa ina visa vya juu vya maambukizi ikilinganishwa na  Nairobi.

Nairobi  inaongoza kwa visa  2,428  ikifutwa na Mombasa kwa visa  1,304. Kaunti za Busia  na  Kajiado  ambazo zina visa vingi kutokana na uwepo wa madereva kutoka nchi jirani zina visa  361  na  179  mtawalia.

Kulingana na  Mwangangi,  licha ya Mombasa kuwa  ya pili kwa idadi ya visa  ina uwezo mkubwa wa maambukizi kwa asilimia  107.9 ikifuatwa na Nairobi kwa asilimia  55.2 kwa kila idadi ya watu laki moja.

Mwangangi amesema Kenya ndio nchi pekee  inayotumia utaratibu wa kuwapa utunzi na matibabu wagonjwa wa corona wakiwa nyumbani kama njia moja ya kupambana na virusi hivyo.