Usikose game ya Arsenal! Mashabiki wamsuta Gidi baada ya kutua London

Siku ya Jumamosi, mtangazaji nguli wa Jambo, Gidi Gidi, alichapisha picha akiwa ndani mwa ndege na kusema kuwa alikuwa njiani kuelekea, London, Uingereza.

Pindi tu alipochapisha, mashabiki wake hawakubaki nyuma kwani wakikumbuka upendo wake Gidi kwa timu ya ligi kuu ya Uingereza, Arsenal, walijua kuwa kuna fursa huenda akahudhuria mechi katika uga wa Emirates.

Ziara ya Gidi inajia wakati Arsenal wanapanga kutifua kivumbi na mahasimu wao wa jadi katika North London derby, siku ya Jumapili mida ya saa kumi na mbili unusu.

Shabiki kwa jina Muge alisema,

Safe travels. Ensure you attend the London Derby on Sunday.

Mwingine kwa jina Varlene hakuwachwa nyuma. Alisema,

 Greetings to Auba n Luca...a win for Arsenal is a win for me👊👊

Siku ya Ijumaa, Gidi alitangaza kupitia mtandao wake wa Instagram, kuwa atakuwa anasheherekea birthday yake katika miji minne mikuu duniani.

Gidi ambaye ameanza likizo yake rasmi anapangia kuzuru London (Labda kutizama mechi ya Arsenal), Paris (Ufaransa), Washinton DC (Marekani) na pia New York City.

Gidi alizaliwa miongo kadhaa iliyopita tarehe 5 Septemba, na kila mwaka yeye huhakikisha kuwa amejivinjari vilivyo lakini kitu ambacho hupenda kufanya ni kusafiri hadi Ufaransa kuitembelea familia yake kwa siku kadhaa.

Mwaka uliopita, Gidi alifanya jambo la busara sana kwani alipanga sherehe ambayo aliwaalika marafiki zake na wakuu kutoka nyanja mbali mbali humu nchini.

Sherehe hiyo iliyo andaliwa katika hoteli ya Ole Sereni, Nairobi ilikuwa na nia moja tu; Kuchangisha fedha za kusaidia wagonjwa wa saratani.

https://www.instagram.com/p/B1zUFCpAa_M/