Usikule vyakula hivi kabla ya ‘pekejeng’

Tendo la ndoa  ni  muhimu kwa wapendanao au wanandoa .Matayarisho mengi tu yanahitajika ili  uweze kumfurahisha mwenzio .Kwa akina dada ,mambo ni mengi na labda umekuwa ukipiga kosa kwa kula  vyakula ambavyo labda vinamsababishia mwenzio  usumbufu au kuwa kikwazo katika kuhakikisha kwamba anakupa raha kamili bila vikwazo .  Imebainika kwamba harufu ya ‘tunda’ la mwanamke huathiriwa na chakula anachokula  na hivyo basi iwapo wataka usitoe uvundo au harufu  ambayo haitampendeza mwenzako basi epuka vyakula hivi

 1.Omena

 Wengi  wanapenda sana  omena  au dagaa ,samakai hawa wadogo ambao pia wamepewa majina mbali mbali majumbani .Nakumbuka kwetu omena hutiwa ‘misumari’. Lakini harufu ya samaki hawa haivutii sana iwapo unajitayarisha kwa  sakato la  utu uzima . Inaarifiwa harufu hiyo inaweza pia kujitokeza katika ‘tunda’ la mwanamke na hivyo basi kuvuruga mazingira ya starehe zeno .Ni bayana pia kwamba harufu ya omena inaweza kusalia kinywani mwako na wakati unampobusu mwenzio ,usimwache katika hali nzuri.

 

  1. Kachumbari

Asiyependa kachumbari ni nani  jamani? Lakini kiungo hiki muhimu katika vyakula vya kawaida kiepuke sana iwapo una mpang wa usiku mzima wa mahaba . Kachumbari ni tamu kweli lakini harufu ya mabaki yake katika kinywa chako sio nzuri endapo unamtaraji mwenzake kujipepesua wazi akikupa mabusu moto moto katika usiku wenu wa raha . Iwapo basi utajipata ushaitumia kachumbari ,hakikisha  umetafuta ‘kifutio’ cha kumaliza harufufu ya mchannganyiko wa vitunguu na  dhania na yote yaliyowekwa katika kachumabari yako .

 Kitunguu saumu

Kumekuwa na dhana ambayo huenda ni potovu kwamba kuweka kitunguu saumu katika uke wako ni tiba ya maambukizi ya ‘yeast’.usisikize hilo kwa sababu halina ithibati ya kiutafiti au matibabu .Kwanza ,kuweka chochote kisicho cha kawaida katika sehemu yako ya siri ni jambo hatari kwa afya yako . Kitungu saumu kina  mvuto wa kipekee katika chakula na ni kiungo muhimu sana kutayarisha mapochpocho pale nyumbani .Lakini ,kama tu uzuri wake ,unafaa kufahamu kwamba kila unachokula kina matokeo yake kwingineko .Harufu ya kitunguu saumu inaweza kujipenyeza na ikaathiri mazingira na harufu yam le ndani . Kwa hivyo iwapo una  misheni ya kujifurahisha bila kizuizi kwa usiku wa  mahaba ,kitunguu saumu kiepuke kama ukoma .Pia unapokila ,kitaacha harufu katika kinywa chako na hutataka kumkaribia mwenzio .

4. Nyama /Red meat

Kula nyama ya Ng’ombe/mbuzi au inayojulikana kama red meat  kunafanya jasho lako kunuka zaidi . Hatua hiyo sasa ndio huenda ikavuruga  mambo yako iwapo umepanga kupiga msakato wa usiku . ‘Glands’ za kutoa jsho katika sehemu mbali za mwili wako zitajiachilia kwa urahisi na kukufanya utokwe jasho wakati umekula nyama .Baadhi ya sehemu za mwili wako zitakazotokwa jasho pia ni sehemu zako za siri !  Kula nyama pia kunajulikana kuathiriwa viwango vya PH katika ‘tunda’ la mwanamke.sehemu hiyo mara nyingi inafaa kuwa na aside kidogo  lakini kuna ushahidi kwamba baadhi ya vyakula kama vile nyama ,samaki vinaweza kueta viwango vya juu vya ‘alkalinity’ na hivyo basi kuvuruga harufu ya ‘tunda’ lako .