Usimuache mpenzi wako! Maono kuwa yeye ndiye mume wako

Wahenga walisema kuwa, mapenzi ni bahari na lipendalo moyo dawa na kwa hakika hawakuwa wanatupaka mafuta kwa mgongo wa chupa kwani ni kweli kabisa kuwa mapenzi ni kitu cha umuhimu sana katika maisha ya binadamu.

Hivyo basi, kama Radio Jambo, tumeweza kuwandalia orodha ya maono ya kuwa huenda uliye naye kwa sasa kama mpenzi wako ndiye atakuwa mume wako.

Ikiwa mpenzi wako hufanya mambo kama haya basi ni yeye! Usimuache hata kidogo.

1.Kama mpenzi wako anakujali.

Ikiwa mpenzi wako hufurahia ama hukufurahia kila wakati kitu nzuri kinatendeka maishanai mwako bali ni yeye mpenzi wako.

Kwani ni wazi kuwa mtu huyu anakupenda kwani hata endapo mambo yako hayafaulu bado atakuwa hapo kukutia motisha.

Zaidi ya hayo, mpenzi huyu hukupa zawadi si tu siku zasherehe za kuzaliwa kwako na siku za krismasi bali wakati wowote.

2.Mpenzi wako anakutakia mema.

Ikiwa mpenzi wako hufurahia sana kuwa karibu nawe hata iwe una familia yako au marafaiki basi ni wazi kuwa huyu ndiye mtu bora kwko kwani anapenda kukaa karibu nawe na hivyo basi atakuwa nawe wakati wowote.
Manufaa ya kupenda kuwa karibu na mpenzi wako ni kuwa utaweza kumjua na utakuwa unampa wakati wa kukuskiza na kuweza kukupa mawaidha ya jinsi ambavyo utafaulu zaidi maishani.

3. Wewe ndiwe Kipaumbele chake

Ikiwa wewe ndiwe kipaumbele cha mpenzi wako basi ni wazi kuwa anakupenda kwani anapowacha kila kitu anachofanya na kukuhudumia ni wazi kuwa wewe ni mtu wa umuhimu sana maishani mwake na pia ni wazi kuwa anajali mahitaji ya moyo wako.

4. Ikiwa hakufichi kwa watu

Ni wazi kuwa mpenzi wako anakupenda na amekuchagua wewe ikiwa anapenda watu wajue kuwa wewe ni mpenzi wake na pia anafurahia sana kuwa nawe maishani mwake.

5. Ikiwa mpenzi wako si msiri.

Jambo moto sana la kujua kuwa mpenzi wako anakupenda na kuwa amekuchagua wewe na hawataki wasichana wengine wengine ni kama, mpenzi wako hana siri.

Ikiwa mpenzi wako ni mkweli na hata hana aibu kuzungumzia uhusiano wake na mabinti wengine basi ni wazi kuwa anataka ujue kila kitu kumhusu.

Zaidi ya hayo, ikiwa mpenzi wako hutimiza kila kitu alichokuahidi na hujaribu juu chini il kusuluhisha tatizo ikiwa kuna matatizo katika uhusiano wenu basi ni yeye mpenzi wako! Usimuache.