‘Usitumie viagra,’ Mike Sonko awashauri wanaume wavivu

Gavana wa kaunti ya Nairobi Mike Sonko aliwashauri wanaume wa humu nchini wachukue fursa ya msimu huu wa baridi kuwapendeza wake zao na hata wapenzi wao katika mahitaji yao au haki zao za kitandani.

Ushauri wake unajiri siku chache baada ya kusherehekea miaka 21 katika ndoa.

"MAKE YOUR GIRLFRIEND/WIFE/PARTNER HAPPY DURING THIS COLD SEASON AND FOR THOSE WITH BIG BELLIES TO ASK FOR MUKOBEROO FROM WESTERN

DO NOT USE VIAGRA AND YOUR MARRIAGE AND RELATIONSHIP WILL NEVER BE THE SAME AGAIN." Sonko Alisema.

Pia aliwaonya wanaume dhidi ya kulewa sana na kushindwa kutimiza mahitaji ya kitandani.

“THIS HABIT OF DRINKING TOO MUCH ALCOHOL AND JUST GOING TO SLEEP MEN SHOULD STOP,”

Kwa kweli Sonko hajawahi kuona aibu ya kuzungumza kilicho akilini mwake na kisha kuwafurahisha mashabiki wake na posti zake zenye ucheshi.

Sonko ni baba wa watoto watano; wasichana watatu na wavulana wawili.