Usivumilie: Sababu Tosha za kuondoka Ndoa isiokufaa

NO MARRIAGE
NO MARRIAGE

Ndoa ama uhusiano kati ya watu wawili wanaopendana na kitu cha kipekee . Ni uhusiano ambao kila mmoja anafaa kumtegemea mwenzake kwa hali na mali na baada ya kuwekeza muda na hisia ili kuhakikisha kwamba mambo yanasonga mbele vyama ,huwa vigumu sana mtu kuamua kusalimu amri na kuondoka uhusiano au ndoa yake .

Lakini kwa sababu ya changamoto nyingi za mahusiano kama vile kutokuwpo mawasiliano yafaayo, ukosefu wa tendo la ndoa , na msaada wa kihisia-kuna sababu ambazo hukufanya useme ‘enough is Enough’ na uondoke .Hizi hapa sababu zinazofaa kukufanya kuacha ndoa au uhusiano wako

  1. Kukataa kuwasiliana .

  Kadri unavyojaribu kuwasilisha ujumbe wako au kuzungumza na mwenzio hataki au hawezi kukuelewa . umejaribu kuzungumza kwa sauti ya chini ,umetoa vitisho  umejaribu kunyamaza lakini hakuna kinachobadiliska .Hii ni ishara kwamba huenda mtindo huo wa malumbano na kutowasiliana ifaavyo ndio utakaokuwa ada . Ishara hii ni mojawapo za kuanza kukutayarisha uzingatie kuondoka.

 2.Kila kitu ni kibaya .

  Hakuna kizuri kinachotoka katika  mdomo wake . unachofanya,unachosema ,unachovalia –vyote havimpendezi! Kama wanandoa au walio katika uhusiano ,panafaa kuwa na njia nzuri ya upedo ya kumwambia mwenzako chochote bila kumkwaza .lakini inafaa kuzua hofu endapo kila anachpofanya au kusema mwenzako kina kuja na  ubaya . tatizo hili linakufanya unakuwa na woga wa kufanya uamuzi wowote ukohofia kwamba majibu ya mwenzako hayayakupendeza na   dhana inayozuka mara nyingi itakuwa ya kudhalilishwa .

 3.Unahisi katika moyo wako kwamba uhusiano huo sio mzuri

  Umefanya kila uwezalo kuboresha uhusiano wako . umezungumza na rafiki zako  na kusoma vitabu viingi kuhusu mahusiano  .katika moyo wako umeshahamu kwamba tayari umebeba mzigo mzito na unakuumiza na huwezi kuendelea hivi .  Msisimko wa kale kati yenu wawili haupo tena . Hali ya uhusiano wenu inazidi kudorora au imesalia pale pale .Hii ni ishara kwamba wakati umewadia kujifungilia mlango na kuchukua basi lijalo .

  1. Kukataa kubadilika/kuboreka

    Hakuna mtu halisi asiye na dosari  .lakini iwapo kuna udhaifu katika mmoja wenu au nyote  basi mnafaa kuchukua hatua za kubadilika ili kuwa watu bora .Chukueni  hatua za kuhakikisha kwamba mnabadilisha mambo ndani yenu ambayo yanavuruga uhusiano wenu .Ila iwapo mwenzio hana nia au ari ya kutaka kubadilika basi itakuwa vigumu kupiga hatua ya kuimarisha uhusiano wenu .

  1. Hataki kupata usaidizi .

Umemrai mwenzako kutafuta  usaidizi wa mshauri ili kumaliza  matatizo ya uhusiano wenu . Labda hata umekuwa wa kwanza kufika kwa mshauri zaidi ya mara moja ukifikiria atategwa na chambo kasha akubali kuja lakini wapi! Kwa ufupi unahisi kuna  hali kubwa  kwa upande wake kukataa kabisa kuja ili kuyaweka wazi masuala ambayo yanavuruga ndoa ama uhusiano wenu .Yeye haoni tatizo lolote ilhali wewe na watu walio nje  wanashuhudia kila kilicho kibaya katika uhusiano huo.

6.Mateso ya kifikra na kupigwa

  Zamani  ilikuwa kawaida wanaume kwa wanawake  kuvumilia ndoa na mahusiano yenye    tatizo kubwa la kusumbuliwa fikra na mwenzako bila kulichukulia kama jambo kubwa .lakini sasa imegundulika kuna uhusiano mkubwa kati ya mtu anayetatizwa fikra na maamuzi anayofanya .Ndoa isiokuwa na kujali ,huzaa maamuzi ambyo huleta kilio . Pia kuna wanandoa –hasa wanawake ambao huvumilia ndoa  licha ya kupigwa na waume zao .Hili halifai kukubalika kwa vyovyote vile na unafaa kufanya uamuzi wa kuondoka uhusiano ama ndoa kama hiyo .

7 .Usinzi/Uzinifu

  Hili halihitaji  maelezo . Ingawaje kuna nyakati mmoja wenu katika uhusiano anaweza kuteleza na kujipata nje ya ndoa , haifai kuwa mtindo wa kumsamhe mwenzako ambaye anahatarisha hali ya uhusiano au ndoa yenu kwa kufanya msururu wa mahusiano ya kimapenzi  na watu wan je ya ndoa .

  Ingawaje  kuna sababu nyingi kuu ambazo zinaweza kukufanya kuondoka katika uhusiano au ndoa ,hizi ni baadhi  tu ya sababu hizo wala sio  msingi wa kuacha ndoa au uhusiano wako . wakati mwingine ,yaweza kuwa sababu moja au mseto wa sababu hizo na nyingine zaidi .  Kwa vyovyote vile ,tumia juhudi zote kuwa na ndoa au uhusiano mzuri lakini usijivunje mgongo  kupasua kuni zisizoweza kushika moto .