Usiyoyafahamu kuhusu Robert Mugabe. Mvaaji wa nguo maridadi sana

25024099_307477449771381_525074762846699520_n__1567835999_92182
25024099_307477449771381_525074762846699520_n__1567835999_92182

Aliyekuwa Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe alifariki dunia akiwa na miaka 95 nchini Singapore. Mugabe alifariki katika hospitali moja ughaibuni alipokuwa akipata matibabu kwa muda mrefu.

Afya yake Robert ilianza kunyong’onyea kwa kipindi kirefu. Wanahabari nchini humo waliwahi kufurushwa wakitaka kumhoji katika hali ya ugonjwa.

Soma hadithi hii :

Alipenda sana suti zinazoutosha mwili wake sawasawa na tai zinazofanana na kitambaa. Kiongozi huyu alikuwa mtu wa kupigiwa mfano mzuri kwa mavazi ya kisasa. Robert aliwavutia sana wanamitindo nchini Zimbabwe kwa mavazi yake.

Soma hadithi hii :

Robert ni kiongozi ambaye hakupenda kushinda kwa lolote. Alipokuwa mchanga, Mugabe alipenda sana kuucheza mchezo wa  tenisi, kwa mujibu wa aliyekuwa mwalimu katika shule ya wakatoliki alikosomea Mugabe. Ila, aliposhindwa katika mchezo huo, aliitupa raketi yake chini kwa hasira.

Rais huyu alipenda sana vyakula vya kiasili na kufanya mazoezi.

Soma hadithi hii :

“Mimi hujihisi mgonjwa wakati sijafanya mazoezi ya viungo vya mwili,” alinukuliwa Mugabe.

Robert alikuwa msomi sana. Mugabe alimiliki shahada 7.  Alituzwa digrii yake ya kwanza kutoka Chuo Kikuu Cha Fort Hare, Afrika Kusini. Kiongozi huyu aliweza kusomea shahada zake nyingine kupitia mtandao akiwa gerezani.Alikuwa na elimu katika nyanja kama sheria elimu, sayansi na usimamizi