utabiri

Utabiri wa mechi katika ligi kuu ya Uingereza

Baada ya mapumziko ya kimataifa yaliyoshuhudia machuano ya kufuzu michuano ya Euro, ligi kuu ya Uingereza imerejea kwa mpigo huku klabu mbali mbali zikitarajiwa kupimana makali kesho jumamosi.

Hapo mwendo wa saa nane unusu, Jurgen Klopp ambaye ni kocha wa klabu ya Liverpool, atakuwa anamenyana na klabu ya Newcastle uwanjani Anfield.

Klabu hii ya Liverpool ilianza msimu huu vizuri kwani hawajapoteza mechi yoyote, huku Newcastle wakitoka sare tasa mechi tatu ambazo Wamecheza wakipoteza moja dhidi ya Arsenali. Je, Newcastle watawabwaga Liverpool?

Utabiri wangu: Liverpool 3-1 Newcastle

MohamedSalah.v.Newcastle

Mwana Manchester United vile vile atakuwa anazamia uwanjani mwendo wa  saa kumi na moja akipambana na Leicester uwanjani Old trafford. Ole Gunnar Solsjaer ambaye ni mkufunzi wa united, alianza msimu vizuri kwa kucharaza Chelsea mabao nne kwa sufuri lakini walitoka sare mechi mbili walizocheza huku Crystal Palace ikiwalaza mabao mbili kwa moja nyumbani kwao. Leicester kwa upande wao wameshinda mechi mbili tangu msimu ulipoanza na vilevile kutoka sare kwa mechi mbili, matokea ambayo si mbaya kulingana na kocha Brendan Rodgers. Aliyekuwa mlinzi wa Leicester Harry Maguire atakuwa anacheza mechi hiyo dhidi ya klabu yake ya zamani. Je, kesho itakuaje?

Utabiri: Man United 1-1 Leicester.

maguirevardy

Tottenham hotspurs watachuana na Crystal palace uwanjani White Hart Lane. Klabu hii ambayo Mauricio Pochettino ni mkufunzi imetoka sare katika mechi mbili, huku wakishinda mechi moja na kupoteza mechi lingine. Crystal kwa upande wao wameshinda mechi mbili na kutoka sare mechi moja huku wakipoteza mechi lingine.

Utabiri: Tottenham 2-1 Crystal Palace.

 

harry kanezaha (1)

Frank Lampard ambaye ni Mkufunzi mpya katika klabu yake ya zamani ya Chelsea, atakuwa na kibarua kigumu wikendi hii kwani atakua anachuana na Wolves uwanjani Molineux. Lampard ambaye alipoteza mechi ya kwanza msimu huu dhidi ya united, ameshinda mechi moja, nakutoka sare katika mechi mbili. Chelsea walipigwa marufuku kusajili wachezaji,lakini Lampard ana imani kuwa timu yake itacheza vizuri huku mshambulizi wao Tammy Abraham akionyesha makali yake kwa kutikisa nyavu mara nne.

Utabiri: Wolves 2-2 Chelsea

 

abuuwolves

Mabingwa watetezi katika ligi hiyo ya Uingereza Manchester City, watakuwa wanashuka uwanjani Carrow road kuchuana na Norwich City. City ambayo iliwacharaza Westham mabao tano kwa bila watakuwa wanazidi kuonyesha makali yao dhidi ya Norwich ambayo imepoteza mechi tatu na kushinda mechi moja. Norwich watakuwa wakitegemea mshambulizi wao Pukki kuwaghadhabisha Mancity, huku mshambulizi huyo akiwa tayari amefunga mabao tano.

Man City 4:1 Norwich.

 

mancitypukki (1)

Siku ya jumapili, vijana wake Unai Emery watachuana na Watford uwanjani Vicarage road. Arsenali ambao wameshinda mechi mbili na kupoteza moja huku wakitoka sare na Tottenham, watakua wanategemea washambulizi wao Aubumeyang, Lacazzette, na Pepe kufanikisha ushindi wao. Vile vile Watford kwa upande wao, wamepoteza mechi tatu huku wakitoka sare tasa na Newcastle. Je, Arsenali watashinda?

pepe-aubameyang-lacazette1deeney070419.1.000

 

 

 

 

 

Photo Credits: sports360, goal.com, skysports ,the telegraph,

Read More:

Comments

comments