eufa europa

Utabiri wa raundi ya pili ya ligi ya Europa, Man United watashinda?

Raundi ya pili ya ligi ya Europa itakuwa inachezwa leo usiku huku klabu mbali mbali kutoka bara hilo wakitarajia kughubia pointi tatu.

Vijana wake Ole Gunnar Solsjaer watakuwa wanasafiri hadi uwanjani Afas Stadion nyumbani kwake klabu ya AZ Alkmaar.

elazalkmaarmanutd031019

Man United ambao walitoka sare tasa na klabu ya Arsenal katika ligi ya Uingereza wiki hii, wanatarajiwa kushamiri katika mechi hiyo ili waweze kuongoza katika kundi hilo, kwani kwa sasa wanashikilia nafasi ya pili na pointi 3 nyuma yake klabu ya Partizan.

Je, unafahamu majina yaliyobandikwa kinara wa ODM Raila Odinga?

 Utabiri wangu ni mwana manchester atamnyuka AZ Alkmaar mabao matatu kwa moja.

Vile vile klabu ya Arsenal watakuwa wanachuana na Standard Liege klabu ambayo inacheza katika ligi ya Ubelgiji.

Unai Emery ambaye ni mkufunzi wa klabu ya Arsenali ana matumaini kuwa vijana wake watashinda mechi hiyo.

elazarsenalstandardliege031019

Kwa sasa klabu hizo mbili zinaongoza katika kundi lao huku wote wakighubia pointi tatu.

Je, nani ataibuka mshindi usiku wa leo?

“Nimerejea katika ubora wangu,” Messi awaambia mahasidi wake

 Utabiri wangu ni Arsenal watashinda mechi hiyo itakayochezewa uwanjani Fly Emirates kwa kufunga mabao 4-2.

Gusa hapa usome hadithi za Abel Omasete

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments