Utafiti waonyesha jinsi wafungwa wanavyotengeza mamilioni jela

unnamed__8___1568014864_37722
unnamed__8___1568014864_37722
Nyuma ya kila mlango wa jela,kuna idadi ya wafungwa 57,000 waliofungiwa baada ya kushtakiwa kuhusika katika uhalifu.

Wapo katika maisha ya upweke. Hakuna familia wala marafiki. Mazingira chafu ya kulala. Vyoo vichafu. Walinzi wakali. Hii ndio taswira ya jela.

Wafungwa walio na kiwango kidogo cha pesa watashawishika kutengeneza hela kibao.

Soma hadithi nyingine:

 Utafiti unabaini kuwa kuna wafungwa katika jela walio katika hali nzuri.

Wale wanajuana na wakubwa wanaishi maisha ya kistaarabu sana. Wana vyoo vya kibinafsi,malazi mazuri,runinga, chakula kizuri au ata vya kunywa.

"Jela kuna vyeo. Kuna una pesa unaishi kistaarabu. Malazi mazuri na unakula chakula kizuri," Anasema mfungwa mmoja.

Vyumba vya kulala jela vina majina ya mitaa hapa jijini.

Soma hadithi nyingine:

 Kuna Runda, Muthaiga, Korogocho and Dandora.

Wafungwa hufanya dili nono zinazoweza kuwachumia 80,000 na 360,000 kwa siku.

Kila uchao,wafungwa wanabuni njia mpya za kuwalaghai watu.

Mfungwa mmoja anasimulia vile wanavyolaghai watu kupitia simu za rununu.

“Ilikuwa rahisi kumdanya mtu kwamba ameshinda zawadi.

Soma hadithi nyingine:

Kitita kikubwa cha pesa tunachokitaja huwa kinamvutia mtu kuamini."

"Ashikapo simu mtu, huwa tunatumia uongo kumdanganya kuwa anazungumza na kituo chetu cha kuwasaidia wateja."

"Hapo tunamueleza kuwa ameshinda milioni 1 kutokana na mjazo wake wa kadi alioufanya."

Soma hadithi nyingine:

 Wafungwa hawa baada ya kukutangaza mshindi, huwa wanaanza hadithi mpya ya jinsi watakutumia hela yako katika akaunti ya benki. Katika zoezi nzima, watamchezea akili mtu ili wapate neno siri ya akaunti ya benki au huduma ya mpesa.

"Wakati huo tuna watu wetu nche ya ATM ya benki hiyo. Wanatoa pesa yote na tunagawana." Asema mfungwa.