Utajua leo iwapo shule zitafunguliwa mapema au mwezi januari

Mkutano utafanyika leo kuamua iwapo shule zitafunguliwa kabla ya januri tarehe moja mwaka ujao .

Shule za kibinafsi na walimu wakuu wanaitaka serikali kuzifungua shule mwezi ujao ili watahiniwa wa KCPE na KCSE waweze kuifanya mitihani hiyo . Januari ndio iliyokuwa imetangaza kwama tarehe ya kufunguliwa kwa shule zote  endapo maambukizi ya Covid 19 yanegekithiri

Mkutano wa leo umeitishwa na waziri wa elimu George Magoha  ambaye ataongoza mkutano wenyewe katika  taasisi ya mtaala wa elimu . Iwapo  pendekezo hilo litakubaliwa basi wanafunzi milioni 1.7 watarejea shuleni .

Muungano wa shule za kibinafsi unataka mitihani ya kitaifa kufanywa kufikia mwezi disemba .

Wanaopendekeza hilo wanasema mtihani sio lazima usheheni  mafunzo ambayo hawakupewa wanafunzi na mtihani wa KCSE unaweza kusheheni tu maswali hadi masomo ya kidato cha tatu .

Mutheu Kasanga,  mwenyekiti wa muungano huo  amesema serikali inafaa kutoa mtihani utakaouliza maswali hadi sehemu waliofika wanafunzi kabla ya janga la corona .

" Shule za kimataifa zilifaulu kuwapeleka wanafunzi wote hadi katika madarasa yafuatayo  bila mtihani . walitumia njia nyingine  ..mbona tufanye mtihani kuwa swala la  maisha na kifo ?’

Ingawaje walimu wengi wakuu wanaunga mkono kufunguliwa kwa shule mwezi ujao wanapinga pendekezo la kufanya mtihani mapema wakisema itakuwa biora kuwatayarisha watahiniwa ili kufanya mtihani mwezi februari mwakani .