Utakulaje chapati na umevalia maski? KOT yamponda Alfred Mutua kuhusu picha mtandaoni

Mutua
Mutua
Mepondwa mitandaoni gavana wa Machakos Alfred Mutua  baada ya picha yake kuwekwa mtandaoni akigawana chapatti na jamaa moja  wakiwa mkahawani  huku wakiwa wamevalia maski .

Katika picha hio ambayo Mutua aliiweka twitter ,watu katika mitandao wameshangaa jinsi wawili hao walivyovalia maski wakikula ilhali watu wengine waliowazigira hawajavalia maski .

Daalili zote zaonyesha kwamba waliipiga picha hiyo katikati ya mlo wao na huenda picha yenywewe ili tu picha-ya kuonyesha walichokuwa wakifanya .

" Nimekuwa nikizungumza na vijana kutumia lugha yao ya mtaani ‘sheng’  na nina video ya kuwahimiza waupuke ukabila na wasije wakawa watazamaji tu katika ulingo wa kisiasa’ Mutua aliandika katika twitter

Haya hapa baadhi ya maoni ya wakenya

https://twitter.com/Trackmann/status/1308798054456324096

https://twitter.com/andama_shadrack/status/1308823166077239297

Siku ya jumatano Mutua alimshtumu kiongozi wa ANC musalia Mudavadi  kwa kuiga mbinu zake za kisiasa . Amesema Mudavadi anazitumia mbinu ake za kampeini inayowalenga vijana kabla ya uchaguzi wa 2022 .

Mutua amesema kwamba katika mwaka mmoja ulioppita amegundua kwamba kila anapoanzisha njia moja ya kufanya jambo kuhusu shughuli zake za kisiasa ,Mudavadi anaiga na kuitumia pia .