Utamaduni huniruhusu kusherekea siku ya wapendanao (Valentine) - Nasra

Ni mwanamke wa kipekee ambaye ni mwislamu na yuko katika sekta ya ucheshi ya Churchchill ambaye anasherehekewa na wananchi wengi kwa ushupavu  wake kwa kuwa katika sekta ya ucheshi.

Nasra hakuweza kuangalia kabila wala kitu chochote cha kumuweka chini bali aliweza kutia bidii katika kazi yake ya ucheshi na sasa ana tabasamu kubwa ya kujivunia kwa kazi yake.

Akiongea katika mahojiano Nasra alisema kuwa motisha wake ni kutoa mawazo ya wanadamu kuwa waislamu ni wabaya.

"Wasomali ni wazuri ambao wanajulikana kwa ukarimu wao, lakini watu wachache wameweza kuweka mawazo katika akili zao kuwa sisi ni wabaya,

"Wamesahau mambo mazuri ambayo huwa tunafanya, naweza fanya jambo nzuri lakini jambo mbaya likitokea wanasahau jambo au mambo mazuri ambayo nimefanya," Alizungumza Nasra.

Nasra alisema kuwa licha ya kuwa mambo yanaenda mzuri na sambamba lakini hupitia changamoto kwa maana yeye ni mwanamke kwa kutengwa.

"Watu hawakupei maadili wala heshima ambayo unastahili kupewa, unaweza itwa kazi pamoja na mwanaume lakini wanatiliwa maanani sana, licha ya kuwa umefanya kazi mzuri na unatia bidii katika kazi kuwaliko,

"Licha ya changamoto ambazo nina pitia uwa nazingatia mambo mazuri," Nasra alieleza.

Wananchi wengi wakisherehekea siku ya wapendanao 14 Februari Nasra hatambui wala kuisherehekea siku hiyo kwa maana hawaruhusiwi wala kukubaliwa na gini pia utamaduni wao.

"Huwa si sherehekei siku ya wapendanao kwa maana utamaduni na dini yangu hainiruhusu, kwa hivyo sitaki kuongelelea sana siku hiyo,"Alisema Nasra.

Kila mtu akiwa katika umri wa Nasra lazima aweze kuwa na mchumba wake, alipoulizwa kama kuwa ana mchumba aliweza kusema kuwa ana mchumba wa Madagascar.

"Nina mchumba ambaye ni mzuri sana kutoka Madagascar, kwa hivo siwezi kuwaidi harusi hivi karibuni kwa sababu wanaume ndio wanapendekeza wanawake (propose),

"Sijui hilo jukumu walipewa na nani, kama wanawake wangepewa jukumu hilo ningepatana na yeye leo na kesho na muoa, saa hii ningekuwa nishaamuoa."Nasra alizungumza.