Utumishi ama ukatili? baadhi ya wanafunzi waliodaiwa kuuawa mikononi mwa polisi

Maafisa wa polisi ni watu ambao wamepitia mafunzo na baadaye kupewa majukumu ya kuhakikisha kuwa wanainchi wanapata usalama wa kutosha.

Lakini kinaya kilionekana hivi maajuzi baada ya video iliowanasa polisi wakimpiga mwanafunzi wa chuo kikuu cha JKUAT kusambaa katika mitandao ya kijamii, tukio ambalo iliwaghadhabisha wakenya wengi.

 Sio mara ya kwanza maafisa wa polisi wametuhumiwa kutumia nguvu kupita kiasi, swali likibakia je, ni hatua gani zilizowekwa ili kuhakikisha kuwa mtu yeyote yule hapitii ukatili huo?

Hawa ni baadhi ya wanafunzi ambao walijeruhiwa na hata kuaga dunia kutokana na maadai ya ukatili kutoka kwa maafisa wa polisi.

1.Carilton Maina

Mnamo Disemba 21, Maina alikuwa anarudi nyumbani baada ya kutoka kutazama mpira kule eneo la laini saba mtaani Kibera. Ni wakati huo ambapo alikumbana na mauti.

Maina alikuwa mwanafunzi katika chu kikuu cha Leeds.

2.Evans Njoroge

Njoroge alikuwa kiongozi wa wanafunzi katika chuo kikuu cha Meru.

aliuawa mnamo Februari 27 wakati wanafunzi wa chuo hicho walikuwa wanaandamana.