Victor Wanyama Azungumzia Swala La Marupurupu Ya Wachezaji Wa Harambee Stars

IMG_0262
IMG_0262
Nahodha wa timu ya taifa Victor Wanyama alizungumzia maswala kadha wa kadha wakati alipozuru studio za Radio Jambo siku ya Jumanne.

Mojawapo ya hayo maswala ni swala la marupurupu ya wachezaji wa timu ya taifa ya Harambee Stars kila wanapokutana kambini katika matayarisho ya mechi za kirafiki na pia za mashindano.

Huku bwana Ghost Mulee akifichua kuwa wachezaji wanalipwa mia saba pekee kwa siku kinyume na elfu tano ambazo walikuwa wanalipwa, wakti alipokuwa kocha wa timu ya taifa, Wanyama hakuwa na budi ila kuthibitisha hayo.

Wanyama aligusia swala la umahiri wa Gor Mahia baada ya msikilizaji kulalamika kuwa timu hiyo yafanya vyema kuliko Harambee Stars.

Nafikiria Gor Mahia ni klabu ambayo imejiwekeza vizuri, kabla wanunue mchezaji wanaangali profile. Wanajua kusajili. Halafu pia wamekuwa wakifanya vizuri kwa hiyo pongezi kwao. Alisema kiungo huyo wa kati wa Tottenham Hotspur.

Halafu timu ya taifa tuna wachezaji wengi tofauti ambao tunapatana kwa mda mfupi wengine wanatoka Gor Mahia, wengine timu zingine. Kwa hivyo ni kujituma tu.

Pesa imepungua ni ukweli so hiyo ndio nilikuwa nasema motivation ikuwa poa hapo ndio wachezaji wataanza kujituma lakini pia sio eti hiyo iwe sababu.

Lakini lazima kwanza tujitume ndio hiyo ingine ije baadaye, naamini tukitia bidii na tujitume na nidhamu iwe juu tutarudi mahala tulikuwa. Aliongeza Wanyama. Aliongeza Wanyama.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be