Victor Wanyama kusalia Tottenham baada ya uhamisho wake kusambaratika

wanyama
wanyama
Victor Wanyama atasalia Tottenham Hostpur, kwa angalau msimu huu. Nahodha huyo wa Harambee Stars alikua amehusishwa na vilabu kadha ya Uropa huku klabu ya Ubelgiji Brugge ikikaribia kumsajili baada ya kukubaliana mkataba wa pauni milioni 12, ambao kisha ulisambaratika siku ya mwisho.

Wanyama alikua ameripotiwa kupewa mkataba wa miaka minne kuondoka kutoka kwa klabu hio ya North London lakini kwa kupunguziwa mshahara wake wa sasa wa pauni elfu 65 kwa wiki.

Harambee Stars wamepigwa jeki na kuwasili kwa Ayub Timbe kabla ya mechi yao ya kirafiki dhidi ya Uganda wikendi hii.

Timbe aliwasili jana mchana kutoka Uchina anakocheza soka na hakushiriki mazoezi nao jana jioni, lakini atashiriki mazoezi asubuhi ya leo, matayarisho yao yanapopamba moto.

Uganda Cranes wakati huo huo wanatarajiwa kuwasili jijini Nairobi hapo kesho kabla ya kipute hicho uwanjani Kasarani kuanzia saa kumi kamili.

Juventus wamewaacha nje kiungo wa kati Emre Can (EMRI CHAN) na mshambulizi Mario Mand-zukic nje ya kikosi chao cha wachezaji 22 kitakachocheza awamu ya makundi ya Champions League. Chan mwenye umri wa miaka 25, alijiunga na miamba hao wa Italia kutoka Liverpool Juni mwaka uliopita Mand-zukic  mwenye umri wa miaka 33 akiwa amehusishwa na kujiunga na Manchester United. Nahodha Giorgio Chiellini pia atakosa kutokana na jeraha la goti. Meneja Maurizio Sarri amewajumuisha wachezaji sita wapya akiwemo Aaron Ramsey.

Wizara ya michezo imetoa mwongozo mpya wa jinsi ya kulipwa kwa wanariadha wanaoiwakilisha Kenya katika mashindano ya kimataifa.

Mwongozo huo unanuia kuhakikisha uwazi, uwajibikaji na ufanisi. Chini ya muongozo huo, itachukua masaa 48 kutoka wakati shirikisho au kamati za kuandaa zitakapowasilisha orodha zao kwa wizara hadi watakapopokea pesa ambazo zitatumwa moja kwa moja kwa akaunti za wanariadha.

Timu zote zitatakiwa kuwasilisha orodha zao siku 14 kabla ya kusafiri huku wanariadha wakilipwa kwanza na wasimamizi wakilipwa baada ya mchakato huo.

Timu ya voliboli ya kinadada itaanza kambi yao ya mazoezi ya siku 6 hii leo uwanjani Kasarani.

Timu hio chini ya ukufunzi wa kocha Paul Bitok itakua inajitayarisha kwa kombe la dunia la FIVB huko Japan itakayoandaliwa katika kipindi cha wiki mbili. Malkia strikers wanatarajiwa kuondoka kuelekea Tokyo jumatano wiki ijayo.