(+Video ) Boni Khalwale shujaa wa kurusha mawe, achangamsha Twitter

unnamed__1573200530_91284
unnamed__1573200530_91284
Wakenya katika mitandao ya kijamii wamemtania aliyekuwa seneta wa Kakamega Boni Khalwale baada ya kuonekana amejihami kijasiri na silaha za mawe jana.

Picha za mwanasiasa huyu ziliteka mitandao yote na kuwafanya watu kuzungumza sana.

Ni kati ya viongozi waliojipata taabani kutoka kwa kero la raia Kibra.

Huenda kitendo cha kushika mawe ni ishara ya kujihami kutokana na vijana waliokuwa na ghadhabu kwa sababu ya visa vya hongo kutolewa mtaani huo.

Khalwale alikuwa amefika katika vituo cha kupiga kura ili 'kulinda' kura za Mariga katika kiwanja cha DC.

Tazama jumbe ;

https://twitter.com/orwaokinda/status/1192504039835090944

https://twitter.com/ItsJeffreyJeff/status/1192477088881741825

Baadaye video imesambaa yake Boni akikwepa kikosi cha vijana waliodai kulinda 'Bedroom ya Baba' katika eneo la Mashimoni.

Farasi wa Boni Khalwale Mariga amekubali kushindwa.

Akimpa kongole mpinzani wake wa karibu Imran Okoth, Mariga amesema ameridhishwa na jinsi uchaguzi huo ulivyoendeshwa.

Ushindi wa mwaniaji wa ODM Imran Okoth katika uchaguzi wa Kibra haufai kuwagawanya wakaazi wa eneo hilo. Viongozi wa ODM Ochillo Ayacko na Mohamed Sumra wanasema ingawaje kulikua na makosa ya uchaguzi, chama chao kinajitahidi kuheshimu maridhiano na uwiano.

IEBC imetakiwa kujitahidi zaidi katika kuhamasisha watu kuhusu umuhimu wa kujitokeza wakati wa chaguzi ndogo. Mkurugenzi wa shirika la HAKI Africa Hussein Khalid anasema katika chaguzi hizo chini ya nusu ya idadi ya watu hujitokeza kupiga kura.

Pia anataka adhabu kali kutolewa kwa wanaojihusisha na makosa wakati wa uchaguzi.