(+ Video) Citizen TV yampata kijana 'ripota' baada ya video yake kusambaa

Screenshot_from_2019_11_02_12_27_38__1572686915_21587
Screenshot_from_2019_11_02_12_27_38__1572686915_21587
Mitandao ya kijamii imesaidia pakubwa katika juhudi za kumpata kijana ambaye alionekana katika video akiripotia kituo cha runinga cha Citizen.

Katika ujumbe wa Twitter, Linus Kaikai ambaye ni mkurugenzi wa stratejia na uvumbuzi katika kampuni ya Royal Media Services amefunguka kuwa wamepata kijana huyo.

https://www.instagram.com/p/B4W4V46Avti/

"WE’VE GOT HIM!  has traced this talented secondary school student. Asanteni nyote." Alichapisha Linus.

Katika video hiyo,kijana huyu anaonekana akiripotia Nimrod Taabu akiwa maeneo ya Narok.

Anachoripoti ni shughuli ya kuwafurusha raia wanaoishi msitu wa Mau.

Serikali ina mipango ya kuhifadhi sehemu hii dhidi ya ukataji miti ovyo kutokana na mijengo na ukulima unaofanyika na raia.

Je, kuna uwezo Citizen TV ikamchukua kijana huyu na kumpa ajira?