mulee viatu

VIDEO: Ghost afichua kuwa bei ya kiatu alichopewa ni sawia na kodi yako!

Bwana Ghost Mulee ni gwiji wa kadanda humu nchini na katika fani yake yeye amefanya urafiki na ma gwiji wengi kutoka nyanja mbalibali, humu nchini na hadi ng’ambo.

Miongoni mwa marafiki hao nikutoka nyanja ya riadha na marafiki wake wa dhati ni Asbel Kiprop na Elijah Manang’oi ambaye ndiye anashikilia ubingwa wa mbio za mita 1500 za Commonwealth na pia ubingwa wa Africa nzima.

Hivi juzi akiwa katika harakati zake za kadanda, bwana Ghost Mulee alipatana na Manang’oi na gwiji huyo akamtunuku viatu murwa kabisa vya riadha kutoka kampuni ya Nike.

Katika mahojiano yetu na Mulee, alisema kuwa aliguswa na ukarimu wa Manang’oi huku akifichua kuwa kiatu kile ni cha zaidi ya shilingi elfu nane.
Manang’oi amekuwa rafiki yangu kwa mda mrefu sasa na nimekuwa nikimuunga mkono, kwani napenda riadha na roho yangu. Mara ya kwanza ilikuwa Asbel Kiprop na sasa Manang’oi ndiye gwiji na nampenda kwani ameshikilia rekodi karibu zote. Ghost Mulee alisema.
Aliongeza.
Baadhi ya rekodi hizo ni kama Commonwealth na pia ubingwa wa Africa nzima. Kwa hivyo alikuja kwa ofisi zetu wakiwa na Cheruiyot bingwa mwingine wa riadha na wote ni wanyenyekevu na hawana mambo mob.
Je anahisi vipi kuhusu kiatu alichozawadiwa?
Hicho kiatu hata sijakivaa hadi naogopa kukipima, in fact nataka kuweka video nikivaa na ilikuja hadi na nyong’onyo (soksi).” Sitakuambia bei yake lakini ni zaidi ya dollar mia nane lakini Manang’oi mungu aibariki roho inayopeana. 
Tazama mahojiano yetu na Mulee karika kanda ifuatayo.

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments