Video hii ina nembo ya lebo yake ya Konde Gang tofauti na kazi za awali zilizokuwa na nembo ya WCB.
WCB inayoongozwa na Diamond imemlea na kumkuza Harmonize.
https://www.instagram.com/p/B5mjx1Ong_k/
Idea au concept ya video inaonekana kufanana na ya Baba Lao ya Diamond Platnumz.
Katika video ya Harmonize, kuna sehemu na ambapo yupo katikati mwa watu waliojifunga buibui nyeusi.
Video ya Baba Lao ilitangulia kudondoka huku Diamond Platnumz akionekana kati ya watu waliovaa suti na kujifunga vitambaa vyeupe.
Magix Enga hatimaye alitangaza kumsamehe.
Akichapisha ujumbe kwenye Insta, Enga alitangaza kuwa walimaliza tofauti zao.
Kuna uwezekano pande mbili zilipatana baada ya ubishi kuwepo kuhusu mdundo wa ngoma hiyo.
https://www.instagram.com/p/B5YZtzMpKLK/
Yote tisa, concept ni ileile.
Sio mara ya kwanza Konde Boy kutuhumiwa kumuiga Diamond ata jinsi anavyoimba na kunengua katika video zake.