(+ Video) Kero kwa Zari The Boss Lady ,Diamond Platnumz na Tanasha kwenye penzi moto

Screenshot_from_2019_12_10_10_08_38__1575961751_54232
Screenshot_from_2019_12_10_10_08_38__1575961751_54232
Msanii wa kizazi kipya Diamond Platnumz amechapisha video katika mtandao wa Insta akionyesha mapenzi ya dhati akiwa na mrembo Tanasha.

Mondi amekuwa katika shughuli za tamasha na kwa hivyo hawajakuwa karibu na mama mtoto kwa siku kadhaa.

Video hii inaonyesha kuwa wawili hawa hawako tayari kuachana na kuwa penzi litazidi kuwaka na kurindima moto zaidi.

https://www.instagram.com/p/B525Ys4Abvs/?utm_source=ig_embed&utm_campaign=embed_video_watch_again

Diamond si mgeni katika maswala ya mahusiano.

Mahusiano yake na Zari The Boss Lady yalikatika baada ya staa huyu kukiri kutoka kimapenzi na Hamisa Mobeto.

Baadaye Hamisa Mobeto aliweza kumburuza mahakamani ili awajibike katika malezi ya mtoto.

Kwa ishara ya video hii, wawili hawa wanaonyesha ishara za kutoachana kamwe.

Wanandoa hawa wana mtoto mchanga ambaye alizaliwa siku sawa na ya babake Diamond Platnumz na kuitwa Naseeb Jnr.