(+ Video) Makovu ya kupoteza kazi Sportpesa, mama aangua kilio Twitter

EF7zIJ2WoAAMzy_
EF7zIJ2WoAAMzy_
Mama mmoja ameteka anga za mtandao wa Twitter baada ya video yake kuchapishwa akifoka maneno ya uchungu baada ya kupoteza kazi yake.

Haya yanajiri muda mchache baada ya kampuni ya Sportpesa kulazimika kutamatisha mikataba ya wafanyikazi 400 kufuatia hatua ya kampuni hiyo kusitisha oparesheni zake nchini Kenya.

Soma hadithi nyingine;

Ronald Karauri, aliwapa wafanyikazi wake taarifa hiyo huku akionekana kujawa na huzuni mwingi.

https://twitter.com/papa_rais/status/1179686181572939777

Katika video kwenye mitandao ya kijamii, wafanyikazi wanaonekana wakiwa wameketi huku Karauri akitoa hotuba yake.

Soma hadithi nyingine;

"Hii sasa watufikirie. President afikiwe na ujumbe....Deputy president na President watufikirie."

'TumekasirikaTumechoka na tumechoka kabisa."

"Siku ingine watatuitaji. Wajue wembe ni ule ule.'

https://twitter.com/papa_rais/status/1179685422731018240

"Ee tumekasika..."

"Mwisho huu wa mwezi kazi yangu imeisha. Mimi ni mama, kodi ya nyumba zinanisubiri ila kazi yangu imeisha...'

Mmoja wa wafanyakazi mmoja amesema kwamba amelazimika kutafuta nyumba ya kodi ya chini kutokana na kitendo cha kufutwa kazi.

Sportpesa Kampuni ilitangaza kusitisha operesheni zake nchini.

Soma hadithi nyingine;

Kupitia kauli kwa vyombo vya habari,  kampuni hii ilisema kwamba itarejelea operesheni zake nchini wakati serikali itakapoweka “mazingira bora ya kuendesha shughuli zao na kuzingatia sera bora za kulipa kodi”.

Tangazo hilo lilijiri saa chache baada ya kampuni ya pili kwa ukubwa wa kamari nchini Kenya Betin, kutangaza kuachisha kazi wafanyikazi wake wote baada ya kusitisha operesheni zake nchini.

Hii inatokana na hatua ya serikali kuanzisha kodi ya asilimia 20 kwa pesa zote mtu anazoshinda, hatua ambayo Sportpesa ilisema inamdhalilisha mteja wao.