VIDEO: Mchezaji Wa Tanzania, Mrisho Khalfan, Afariki Baada Ya Kufunga Bao

ismail-mrisho
ismail-mrisho
Kinda wa Mbao FC ya Mwanza, Ismail Mrisho Khalfan amefariki dunia leo baada ya kuzirai uwanjani alipogongana na beki wa Mwadui FC katika michuano ya Ligi ya Vijana wasiozidi umri wa miaka ishirini inayoendelea.
Kulingana na , mechi hiyo ilipigwa kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba na juhudi kubwa zilifanyika kuokoa maisha ya mchezaji huyo, bila mafanikio.
“Inaonekana alishafariki dunia pale uwanjani, tulifanya juhudi kubwa mimi na wenzangu. Tulisaidiana na watu wengine pia waliokuwa uwanjani, lakini ilionekana hakukuwa na majibu mazuri,” alisema mmoja wa madaktari waliojaribu kuokoa maisha ya kijana huyo.
Mwenyezi Mungu Amrehemu.
Tazama kanda ifuatayo...