VIDEO: Msanii Eric Omondi Anapeperusha Bendera Ya Kenya Kimataifa - Propesa

eric-omondi
eric-omondi
Hivi majuzi, msanii Eric Omondi ambaye anajulikana sio Afrika pekee bali duniani kwote kwa utumbuizaji wake amezidi kupokea sifa kutoka nyanja zote, baada ya msanii huyo kuingia katika kumbukumbu alipopata fursa ya kutumbuiza watazamaji katika kipindi maarufu chake Jimmy Fallon, cha 'The Tonight Show' msanii maarufu zaidi duniani.

Hayo yalitendeka wiki iliyopita mjini New York na wakenya kutoka tabaka mbalimbali walimpa kongole bwana Omondi kwani ni ndoto ya kila mmoja kuweza kupiga hatua kimataifa.

Baadhi ya waliompongeza Eric Omondi ambaye kitambo alikuwa msanii katika kipindi cha Churchill Show, ni wasanii wenzake wakiwemo kikundi cha Propesa.

Kulingana na Propesa, hatua aliyopiga msanii huyo si yake pekee bali alipeperusha bendera ya Kenya kimataifa kwani ilikuwa ni ishara tosha kuwa pia wasanii wa Kenya waweza tawala nyanja mbalimbali ikiwemo sanaa.

"Eriko anawakilisha Kenya humo nje, hajifanyii mwenyewe wala mrembo wake bali ni sisi sote na tunampongeza sanasana. " Walisema Propesa ambao walifichua kuwa msanii huyo ni mmoja wa wale wamekuwa nguzo kuu katika maisha yao haswa walipokuwa wakianza usanii.

Tazama kanda ifuatayo.