VIDEO: Nyce Wanjeri na marafiki zake wahakikisha kuwa 'Nobody can stop reggae'

Msemo wa 'no one can stop reggae' au 'reggae cannot be stopped' umekuwa ukitumiwa sana kwa muda. Ni msemo ambao ulitokana na wimbo maarufu wa reggae ujulikanao kama 'Reggae Strong' wimbo ulioimbwa na msanii Lucky Dube.

Msemo huo umekuwa ukiongezewa nguvu na umaarufu mwingi humu nchini na kiongozi wa ODM, Raila Odinga, kwani amekuwa akiutumia zaidi katika pilkapilka zake za mikutano ya BBI, nchini kote.

Tangia ugonjwa wa Coronavirus uingie nchini na kusitisha shughuli zote za wakenya, wengi walikubaliana kuwa, hatimaye reggae imesimamishwa, jambo ambalo halikuwahi sikika.

Hata hivyo, huku tukikosa yeyote wa kufufua reggae na kuendeleza msemo huu nyakati hizi, muigizaji Nyce Wanjeri na genge lake la wasichana maarufu na wenye talanta chungu nzima waliamua hawatotizama huku reggae ikididimia.

Wanjeri akishirikiana na Jackyvike, Shix Kapienga, Sandra dacha, Teacher Wanjiku na Nyamide, wasichana hao walipeperusha bendera ya reggae juu katika mtindo unaopamba moto wa  'Don't rush challenge.'

Tazama video hii ambayo itakuacha kinywa wazi;

https://www.instagram.com/tv/B-xHuJsnwDj/?igshid=1uqsh9hqiazqd