VIDEO: Uhuru Kenyatta Azungumza Na Mbusii Na Lion Deh Kuhusu Mipango Yake Kwa Kina Mama

mbusii.000.uhuru
mbusii.000.uhuru
Miezi kadhaa baada ya kumualika mtangazaji Mbusii katika ikulu ya Nairobi, rais Uhuru Kenyatta alipatana tena na mtangazaji huyo wa Mbusii na Lion Teketeke na kumpa fursa ya kumhoji.

Rais Kenyatta alikuwa katika pilkapilka za ziara ya kampeini katika maeneo ya Isiola na Meru na hapo akawapa wanahabari fursa murwa ya kumhoji, huku Mbusii na Lion deh wakiwa miongoni mwao.

Akizungumza nao, Kenyatta aligusia mengi kuhusu vijana na kina mama, pindi tu atakapochaguliwa kwa mhula wa pili ifikapo tarehe nane mwezi wa Agosti, 2017.

"Kina mama ambao hawana mabwana sijaskia ukisema mipango yako kwao, je umewapangia yepi?." Aliuliza Lion Deh.

"Sisi mipango yetu ni ya kina mama wote ndipo tunasema watajifungua bure katika hospitali zote.

Ndio twasema tutawapatia kadi za bima ya hospitali ya NHIF pindi tu wanapojifungia ili mama au mtoto atakapo kuwa mgonjwa atatibiwa kwa urahisi, iwe mama mwenye bwana au la wote ni mama zetu na tunataka tuhakikishe yakwamba wamehusishwa na wamechungwa na serikali yao kama wale wengine wote." Alisema Rais.

"Halafu sasa Orezo mayoutman wanauliza ukichaguliwa tena utawafanyia nini katika siku tisini za kwanza?." Aliuliza Mbusii.

"Tumesema ya kwamba tunataka kuhakikisha ya kwamba vijana wetu wote tumeweza kupanua mradi wetu wa fedha za vijana ambao umesaidia watu wengi zaidi. Kwa wale ambao wamepata uzoefu katika mipango yetu ya mafunzo ya vijana baada ya kumaliza shule.

Kama hawatapata kazi basi watakopa zile fedha na kuwawezesha kufungua kazi na biashara zao. " Alijibu Kenyatta.

Pata mahojiano yote moja kwa moja katika kanda ifuatayo.