Video ya siku: Mashabiki wa Man U humu nchini waiombea timu yao mlimani

mashabiki wa man united
mashabiki wa man united
Siku ya leo katika ligi kuu ya Uingereza, kuna mechi bomba kabisa ambayo inatazamiwa na mashabiki wengi duniani. Mechi hii ni dhidi ya Manchester United na Manchester City, al maarufu, Manchester derby.

Mechi hii kama ilivyo desturi huwaleta wapinzani hawa wakuu kutoka mtaa wa Manchester na kila wakati huwa ya kusisimua zaidi.

Manchester City ambao ni mabingwa kwa mika miwili sasa hawajakuwa wakionesha mchezo bora kama misimu iliyopita na wanashikilia nafasi ya tatu nyuma ya Leicester City, na wako nyuma ya viongozi Liverpool kwa alama 11.

United kwa upande wao walionesha ubabe wiki hii baada ya kumuadhibu aliyekuwa kocha wao, Jose Mourinho 2-1 alipoiongoza Tottenham hadi Old Trafford.

Hii ikiwa mechi kuu, mashabiki wa Kenya wa Man U wakiongozwa na mcheshi Eric Omondi wamechukua hatua ya kuiombea timu yao ili waibuke washindi baada ya kuwa na msururu wa matokeo mabaya.

Kanda hii imesambaa sana duniani na inawafurahisha wengi haswa mashabiki wa Red Devils.

Tazama kanda hii,

https://twitter.com/TrollFootball/status/1203039396875755521