(+VIDEO)Rayvanny azungumzia mipango ya kutoka WCB

Msanii wa bongo Shaban Mwakyusa almaarufu Rayvanny amekana madai kuwa anatengana na msanii Diamond Platnumz na kutoka katika lebo ya Wasafi.

Rayvanny alikana madai hayo alipokuwa na mazungumzo na mashabiki wake katika runinga ya wasafi, mmoja wa mashabiki wake alikuwa na haya ya kumuuliza.

“Kwa mfano sasa hivi inatokea unaambiwa sasa hivi kuwa unahama label ya wasafi, Label gani nyingine ambayo unahisi unaweza ukaenda?"

Msajiliwa huyo wa WCB alisema kuwa hatoki katika lebo hiyo hivi karibuni na kama ni kutoka katika lebo ya WCB atakuwa ameenda kufungua lebo yake.

“Before sijaongeoa chochote, Vanny Boy, Wasafi for Life Beiby. Kwanza nisema naishukuru sana Management yangu, WCB Wasafi, Namshukuru sana Diamond Platnumz kwa sehemu niliyofika. Nikiamua kuwa na label, naweza hata kuwa na label hata tano. So there is no way kwamba nitoke Wasafi alafu niende kuwa chini ya Label nyingine, Labda niwe na label kumi zingine za kwangu mimi." Alisema Rayvanny.

Rayvanny ameimba nyimbo nyingi akimshirikisha Diamond, alisajiliwa katika lebo hiyo mnamo mwaka wa 2015 na kisha kuutoa wimbo wake wa kwanza mwaka wa 2016.

Msanii huyo ameshinda tuzo kadhaa katika sanaa ya muziki.

Hii hapa video yake;