Vijana wanaounga Jubilee mkono waahidi kumpigia debe Imran Okoth

Imran Vs Mariga-compressed
Imran Vs Mariga-compressed
Kundi la vijana wanaounga  mrengo wa Jubilee waahidi kupigia debe mwaniaji wa chama cha ODM Imran Okoth, katika uchaguzi mdogo wa  eneobunge la Kibra.

Vijana hao wanasema wanafanya hivyo kama ishara ya  maridhiano na kukumbatia wito wa 'Handshake' baina ya Rais  Uhuru na Raila Odinga.

"Tutawahamasisha vijana na wanachama wenzetu wa chama cha Jubilee kuunga mkono, kupigia kura na kulinda kura za Imran Okoth wa ODM. Kibra ipo salama mikononi mwake na wito wa "Handshake" utasalia kuwa imara zaidi, " Zack Kinuthia alisema.

Kinuthia alisema kuwa kikundi hicho kitamuunga mkono Rais Uhuru Kenyatta na Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga katika kueneza "Handshake" na maridhiano  huko Kibra na kote nchini.

Uhuru na Raila walikumbatia wito wa "Handshake" Machi 9 na kumaliza uhasama ambao ulitangulia uchaguzi mkuu wa 2017.

Miongoni mwa waliokuwepo kuwapokea vijana hao ni pamoja na kiongozi wa walio wachache katika bunge la kaunti ya Nairobi Elias Otieno na naibu wa gavana wa zamani wa Kisumu, Ruth Odinga.

Otieno aliwashukuru vijana hao kwa kumuunga mkono mgombeaji wa ODM na na wito Handshake.

"Kibra ni eneo la ODM. Sisi, hata hivyo, tunataka kufahamu ukweli kwamba wapinzani wetu walitaka kushiriki kwenye kinyang'anyiro hiki, ambazo hazingekuwa za kupendeza bila uwepo wao, ”alisema.

Odinga aliwashukuru vijana hao kwa kuchukua hatua ya ujasiri na kumuunga mkono Imran.

"Inatia moyo kuona vijana ambao wako madhubuti. Handshake imeleta amani na na kile wanachofanya vijana hawao tu kitaimarisha zaidi, " Raila alisema.

"Tutakwenda mlango kwa mlango. Kanisa kwa kanisa katika kampeni ambayo haijawahi kushuhudiwa hapo awali, "Kinuthia alisema.

Vijana hao wanadai kwamba Rais Uhuru hakumuunga mkono Mariga kikamilifu katika ugombeaji wa kiti hicho.

"Rais alimwita tu katika Ikulu na hakuwahi kusema chochote isipokuwa kupiga picha na Mariga," Kinuthia alisema.