Vijimambo vya dunia! Wanawake wawili wauawa baada ya kuonekana wakimbusu mwanamume

Pakistani
Pakistani
Katika tukio lisilo la kawaida, wanawake wawili katika taifa la Pakistan wameuawa kinyama baada ya video kuenea mitandaoni wakimbusu mwanamumu. Mabinamu hao wa miaka 22 na 24 walipigwa risasi na kuzikwa Mei 14 katika vitongoji vya Pakistani eneo la Waziristan, taarifa ambazo zimethibitishwa na mkuu wa polisi  Muhammad Nawaz Khan.

Khan, baba mzazi wa mmoja wa mwathiriwa na ndugu ya mwathiriwa mwingine walitiwa mbaroni Jumapili na kukiri kuwa waliwaangamiza wanawake hao.

Maeneo ya Kaskazini na Kusini mwa Waziristan katika taifa la Pakistan yanajulikana sana kutokana na sheria za udhalimu, wanawake hawaruhusiwa kutoka nje ya nyumba bila kuandamana na mtu mwingine, mienendo ya kifamilia inatathminiwa na tabia za mwanamke, kulingana na ripoti ya shirika la kutetea haki za binadamu  Amnesty International.

Katika taarifa yake, Human Rights Watch imesema kuwa watu wengi waliokashifu mauwaji hayo katika mitandao ya kijamii katika taifa hilo maisha yao sasa yamo hatarini na wameitaka serikali kuwahakikishia usalama wao.

“The local administration must take all possible steps to ensure the security of the third girl and the man in the video, and to bring the perpetrator to justice,”  limesema shirika hilo.

Pakistani ni taifa la sita ulimwenguni lililo na watu wengi sana japo ni taifa miongoni mwa mataifa ambayo uhalisia wa kijinsia ama (Gender parity) haidumishwi kivyovyote vile huku haki za kibinadamu zikikiukwa kila mara.

MHARIRI: DAVIS OJIAMBO