Athari za Corona; Vinyozi na Saluni zafungwa Mombasa kutokana na amri ya Gavana Joho

81735246_178176286754914_6388411629224402329_n (1)
81735246_178176286754914_6388411629224402329_n (1)
NA NICKSON TOSI

Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho ameagiza kufungwa kwa Vinyozi na Saluni kama njia ya kuweka mikakati ya kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona katika baadhi ya maeneo ya kaunti za Pwani.

Joho alikuwa ametoa wito wa kuwazuia  wananchi kutotoka nje, 'Total lockdown' eneo hilo akihoji ndio njia ya kipekee ya kuzuia virusi hivyo kuenea zaidi katika maeneo ya Pwani baada ya visa vingi kuripotiwa eneo hilo haswa katika kaunti jirani za Kwale na Kilifi.

Mamia ya watu kutoka kaunti ya Kilifi wamewekwa katika uangalizi kwenye hospitali za kaunti ya Mombasa kwa hofu ya kuambukizwa virusi vya Corona.

Uongozi  wa kaunti ya Mombasa pia umeamuru Matatu, Tuk tuk, boda boda na wachuuzi kutoruhusiwa kuhudumu karibu na kivukio cha feri ili kuzuia msongamano wa watu.

Mhariri; Davis Ojiambo