Viongozi Wa ODM Kisumu Wataka Viongozi Kujiepusha Na Matamshi Ya Uchochezi

Viongozi was ODM kaunti ya Kisumu wamewaonya viongozi wenzao kujiepusha kueneza matamshi ya chuki yanayolenga kuligawanya taifa hili kwa misingi ya kikabila.
 
Kupitia kwa mweka hazina wa chama cha ODM tawi la Kisumu ya Kati Edward Ogola, amewashauri wanasiasa kuchunga matamshi yao kila wanapowahutubia wananchi.
 
Ogolla badala yake ametoa changamoto kwa wanasiasa kutumia mikutano ya hadhara kueneza amani na umoja nchini kwa manufaa ya uchumi wa taifa hili.
 
Ameshikilia kuwa umoja na amani ni muhimu zaidi kwa taifa hili hasaa wakati huu taifa linapojiandaa kushiriki uchaguzi mkuu ujao.