Viongozi waliohudumu kama makamu wa rais Moi

Daniel Torotich Arap Moi ni kiongozi ambaye alihudumu kwa muda wa miaka 24 kama Rais wa pili wa jamhuri ya Kenya.

Hii ni baada ya Rais wa kwanza Mzee Jomo Kenyatta kufariki dunia mwaka wa 1978, huku Moi ambaye alikuwa makamu wake akichukua usukani wa kuendesha shughuli nchini Kenya wakati huo.

 Rais Daniel Moi alipohudumu kama Rais kwa zaidi ya miongo miwili, alikuwa na makamu tofauti kama wafuatao;

1978-1988- Mwai Kibaki alichaguliwa kama makamu wa Rais kwa kipindi cha miaka kumi.

1988-1989-  Rais Moi alimchagua Josephat Njuguna Karanja kama naibu wake. Karanja alihudumu kama naibu wa rais kwa kipindi cha mwaka mmoja.

1989-1997-  George Saitoti alichaguliwa kuhudumu kama makamu wa Rais wa tatu wa Rais Daniel Moi.

1999 Aprili-30, Agosti,2002-  George Saitoti alichaguliwa tena kuwa makamu wa Rais kwa kipindi hicho.

4, Novemba,2002-30, Disemba 2002- Wycliffe Musalia Mudavadi alihudumu kwa kipindi hicho kifupi kama makamu wa Rais Daniel Moi.