VIDEO: Evelyn Wanjiru arudi na kibao kipya 'Everlasting'

Evelyn Wanjiru
Evelyn Wanjiru
Image: courtesy

Msanii gwiji, Evelyn Wanjiru amerudi tena na kibao kipya chenye kupapasa moyo kwa jina 'Everlasting.'

Kibao hiki ambacho kimezalishwa na Bwenieve, kina mdundo wa aina yake ambao umehusisha mziki wa ki Afrika na wa Carribean.

Unaposkiza wimbo huu, mwimbaji Evelyn, anaeleza jinisi jamii tofauti duniani kote humuita mwenyezi mungu.

Mziki huu ni wa dakika tatu na Video yake ni ya kuvutia ambayo huku ikionesha mandhari ya nchii hii. 

Kulingana na Evelyn, mandhari hayo yanaonesha maeneo tofauti ya jiji kuu la Nairobi.

Tayari, video hii imevutia watu elfu kumi na tatu katika mtandao wa Youtube.

Tazama video hii;