'Umegeuzwa kuwa benki,'Gidi amwambia mwanamume aliyedai haya

Muhtasari
  • Mwanamume mmoja alieleza masaibu ambayo amekuwa akipitia mikononi mwa mkewe
  • Titus alidai kuwa anataka mke wake amrudishie kila kitu ambacho alimnunulia na pesa zake
  • Mtangazaji Gidi alimpa ushauri na kumwambia kuwa amegauzwa kuwa benki
Gidi na Ghost

Katika kipindi cha Gidi na Ghost asubuhi mwanamume mmoja alipiga simu ili apatanishwe na mkewe ambaye alichukuliwa na dada yake na kupeleka kwao.

Titus alieleza masaibu ambayo amepitia baada ya mkewe kuenda.

"Mke wangu alichukuliwa na dada yake na kumpeleka kwao, waliniambia nimngoje kwenye kituo cha basi lakini hakuwasili kesho yake

Kwa muda sasa nimekuwa nikituma pesa, ananiambia ni za nauli lakini endapo nampigia simu ananiambia kuwa pesa hizo zilipotea au alitoa vibaya zikaenda kwa agenti nyingine ya M-pesa

Nilipomtumia awali aliniambia kuwa ametumia pesa, na napaswa kumtumia pesa zingine." Alieleza Titus.

Mwanamume huyo alizidi na kuzungumza kwa uchungu na kusema;

"Kama ameamua kuniacha nataka kila kitu ambacho nilimnunulia na hata wanirudishie pesa zangu hata za saluni."

Baada ya kufanya juhudi za kumpigia mkewe alizima simu, huku Gidi akimpa mwanamume huyo ushauri.

"Wacha nikuambie kama mwanamume mwenzangu umegeuzwa na kuwa benki." Gidi alimwambia.