Mume wangu alitumia shilingi 400,000 tulizokuwa tumeweka kwa raha, kumuuliza alinimwagia maji-Mwanamke asimulia

Muhtasari
  • Mume wangu alitumia shillingi 400,000 tulizokuwa tumewekeza kwa raha
  • Mwanamke huyo alisema baada ya mwaka mmoja alirudi kwake licha ya yake kuoa mwanamke mwingine na kumfukuza
  • Pia alifichua kuwa yeye ni mke wa nne 
massawe
massawe

Katika kipindi cha 'Bustani la Massawe Japanni'mwanamke mmoja alipiga simu na kueleza masaibu ambayo alipitia akiwa mikononi mwa mumewe.

Huku akieleza jinsi mumewe alitumia pesa walizokuwa wamewekeza, alisema kwamba mumewe alitumia shillingi 400,000 kwa raha na wanawake alipomuuliza mwanamume huyo alikuwa na ujasiri wa kumwagia maji.

"Nilipomuuliza pesa alipeleka wapi aliniambia kuwa anajenga nyumbani ilhali ilikuwa uongo, nilipomuuiza pesa zilienda wapi alinimwagia maji na kunipa elfu mbili akaniambia hizo ndizo pesa zangu

 

Alitoka na kuenda kula raha, alipoenda alioa mwanamke mwingine ambaye wamebarikiwa na mtoto mmoja

Baada ya pesa kuisha alimfukuza mwanamke huyo na kurudi kwangu, nilimkubali tena na sasa tunaishi pamoja

Ata nikiekelea pesa zangu kwa meza hawezi guza." Mwanamke huyo alisimulia.

Cha kushangaza mwanamke huyo alisema kwamba ana miaka 28 huku mumewe akiwa na miaka50.